المدة الزمنية 10:4

SERIKALI KUNUNUA TANI 90,000 ZA MAHINDI KWA WAKULIMA

بواسطة HABARIMPYA TV
842 مشاهدة
0
3
تم نشره في 2021/09/14

WAZIRI wa Kilimo Prof Adolf Mkenda amesema kwa sasa mahindi yatanunuliwa tani 90,000 ambapo Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) utaanza kununua kwenye mikoa saba kwa bei ya sh. 500 kwa Kilogramu huku Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) ikinunua mikoa sita kwa bei ya soko. Alitaja mikoa saba ambayo NFRA itaanza kununua mahindi hayo kuwa ni pamoja na Ruvuma, Rukwa, Njombe, Songwe, Mbeya, Katavi na Iringa huku CPB ikinunua mikoa sita ambayo ni Rukwa, Katavi, Njombe, Songwe, Dodoma na Manyara. Hayo ameyasema jijini Dodoma leo tarehe 14 Septemba 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa mara baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa Tsh Bilioni 50 kwa ajili ya kuiwezesha NFRA kununua mahindi kwa wakulima hasa wadogo. Amesema zoezi la kununua mahindi tayari lilitangazwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya Rais Samia kuidhinisha sh. Bilioni 50 kwa kazi hiyo. Amebainisha kuwa mwaka huu zimezalishwa tani milioni sita za mahindi huku ziada ikiwa mara mbili ya uzalishaji uliofanyika kwa mwama uliopita huku nchi za Zimbabwe, Zambia zikitajwa kuzalisha kwa wingi nafaka hiyo.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0